Kuonyesha Video ( 1076 - 1100 Katika jumla ya: 1290 )
2015-10-20
Kwenye Muhadhara huu kabainisha Sh: Khaled Yasin ya kwamba ni wajibu wetu kuwakinaisha watu kuhusu Uislamu kimatendo, na tusitosheki pekeyake kutoa dalili tu, yatakiwa mifano mbali mbali kama: Biashara ya Riba, kunywa pombe, sigara, madawa ya kulevya, kujitoa muhanga, Uislamu ni Dini yenye ufumbuzi wa yote hayo na matatizo ya maisha kwaujumla.
2015-10-20
Wanatuelezea watu wanne Mpagani mmoja na wakristo wa tatu kuhusu kusilimu kwao muda ulio pita, kwenye kipindi cha (The Deenshow) kisa kifupi na kwamba waliupata Uislamu ndani ya nafsi zao.
2015-10-16
Wanatuelezea ndugu wengi namna walivyo pata njia ya kuelekea ktk Dini ya kweli.
2015-10-13
Maana kwa ufupi kuhusu Dini ya Uislamu. Uislamu ni Dini ya Amani.
2015-10-13
Njia nzuri sana ya kubainisha Uislamu kwa Wakristo kwa njia ya mdahalo kumuelezea Mungu upande wa wakristo.
yote haya yanatimia kwa njia ya upole na kwaadabu.
2015-10-13
Video inamuelezea Mtume (s.a.w), na kubainisha huruma wake (s.a.w) kwa Wanyama.
2015-09-23
Mada hii inazungumzia: Mapenzi ya Allah juu ya waja wake na kwamba siku ya Arafa ni sababu ya waja kurudi kwa Mola wao pamoja na kulia sana, pia imezungumzia siku ya Arafa Allah anakuwa karibu na waja wake.
2015-09-23
Mada hii inazungumzia: Ubora wa siku ya Arafa na kwamba ni siku ya kutubia na kuomba dua pamoja na kufanya tasbihi sana, pia imezungumzia umuhimu wa kuwa na yakini na kuto kata tamaa kwani Rehma ya Allah ni pana.
2015-09-23
Mada hii inazungumzia: Nguzo za Hijja na yaliyo wajibu kufanya katika Hijja, pia imezungumzia aina za Hijja na yanayo fungamana nazo.
2015-09-23
Mada hii inazungumzia: Inazungumzia maana ya Arafa na Aya iliyoshuka kwa Mtume (s.a.w) alipokuwa Arafa, pia imezungumzia Arafa ni siku ambayo watu wanaachwa huru na moto.
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Uzito na ubora wa siku ya Arafa na jinsi inavyo fanana na siku ya Qiyama pia nikwamba mwenye kufanya Hijja anatakiwa akithirishe kufanya toba, pia imezungumzia umuhimu wa kuendelea kufanya matendo mema baada Hijja.
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Mwenye kufanya Hijja azingatie kila kipengele katika vipengele vya Hijja, pia imezungumzia kuchunga matendo ya Hijja, kukithirisha dua pamoja na kukumbuka Akhera (Qiyama)
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Mafungamano baina ya mkusanyiko wa siku za Hijja na siku ya Qiyama, pia imezungumzia anayefanya Hijja akumbuke mnasaba wa kumvisha sanda maiti na uvaaji wa ihram.
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Fadhila za Hijja na mapenzi ya Allah kwa waja wake na kwamba mwenye kufanya Hijja ya kweli malipo yake ni pepo, pia imezungumzia Hijja ni mazingatio kwa waja ili watu wasibaguane na wala wasidharauliane.
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Sehemu zilizo bora na muhimu kuomba dua kwa mwenye kufanya Hijja kama alivyokua akifanya Mtume (s.a.w) na watu wema waliopia, pia imezungumzia umuhimu wa kuchunga matendo ya Hijja na kuto ya changanya na shirki.
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa ukarimu wa Allah ni kwamba Allah anawakusanya mahujjaji wote katika viwanja vya Arafa wakiwa katika vazi la aina moja, pia imezungumzia kuwa pepo ndiyo malipo ya mtu mwenye kufanya Hijja ya kweli.
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa ukarimu wa Allah juu ya wake ni kwamba amempa mwanadamu akili na akamfanya kuwa kiumbe bora kuliko, pia imezungumzia umuhimu wa kufanya toba ya kweli katika masiku ya Hijja
2015-09-20
Mada hii inazungumzia: Maana ya ukarimu na kwamba ukarimu wa Allah unadhihirika pale mwanadamu atakapojiangali namna alivyoumbwa, pia imezungumzia vitu bora alivyo wapa Allah waja wake kwa ukarimu wake.
2015-09-18
Video hii yahusu Kisa cha kuslimu Kohani wa kihindusi, inaelezea sababu iliyo mpelekea kuusoma Uislamu na kuingia, kisha akawa mlinganiaji mkubwa sana.
2015-09-18
Video hii kwa lugha ya Kingereza inazungumzia kisa cha kuslimu Kenneth, na maisha yake bada ya Kuslimu.
2015-09-18
Muhadhara wa video kwa lugha ya kingereza anajibu Dr. Lawrence Brown maswali mazito mazito yanayo umiza kichwa nayo: Nani aliyeniumba? na kwa nini nipo hapa? na nitapokuwa mwema jee hili halitoshi? na kwanini hatuwezi kumuabudu Mungu kwa utaratibu tunaoutaka?.
2015-09-18
Muhadhara mzuri sana ukielezea Mazuri ya dini ya Uislamu, ya kwamba inaongoza jamii kufanya yatakayo waokowa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
2015-09-18
Kaelezea Sheikh kwenye muhadhara huu baadhi ya mambo ya msingi kuhusu Uislamu na Waislamu.
2015-09-17
Mada hii inazungumzia: Hijja ni wito na kwamba ni muhimu kujitahidi kufanya ibada katika masiku ya Hijja nakumuomba Allah sana ili kupata radhi za Allah katika masiku yahija matukufu.
2015-09-17
Mada hii inazungumzia: Siku ya Arafa na fadhila zake na kwamba Hijja haikamiliki bila ya kusimama Arafa na ni siku ambayo dua zinajibiwa, pia imezungumzia umuhimu wa kushukuru neema za Allah.
Go to the Top