Kuonyesha Video ( 926 - 950 Katika jumla ya: 1096 )
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake29
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) juu ya malipo ya mtu mwenye kwenda mapema msikitini, pia imezungumzia faidha ya swala ya jamaa na umuhimu wa kukumbuka neema za Allah kabla ya kuulizwa siku ya Qiyama.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 28
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Umuhimu na ubora kwa mwanamke wa kiislamu kuswalia nyumbani, pia imezungumzia fadhila anazopata mtu anapokaa msikitini akisubiri kuswali.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 27
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) juu ya ubora na thawabu anazopata mtu anapoenda msikitini, pia imezunguzia hatari ya mwanaume wa kiislamu kuswalia nyumbani badala ya msikitini.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 26
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa faida za kumtembelea mgonjwa au ndugu katika Uislamu ikiwemo kukumbushana katika mambo ya kheri, pia imezungumzia umuhimu na ubora wa ibada ya swala.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 25
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika kuwalea mabinti katika majumba na malipo anayo pata mwenye kuwalea mabinti wawili katika misingi ya uislam, pia amezungumza kuwa watoto wakike wanalindwa.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 24
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Adabu za kumtembelea ndugu katika Uislamu na namna ya kumuandalia mgeni chakula, pia imezungumzia umuhimu wa mzazi kuwalea watoto katika malezi bora ya kiislamu.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 23
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Sababu ya Qabil kumua ndugu yake Habil na namna alivyomzika, pia imezungumzia hatari ya dhambi ya kuua na umuhimu kwa muislamu kujutia madhambi.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 22
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Miongoni wa sababu za mtu kuokoka na Moto wa Jahanam, pia imezungumzia umuhimu wa kutoa kilicho bora kwa ajili ya Allah na hatari ya ubakhili na imeelezea kwa ufupi kisa cha watoto wa Nabii Adam (a.s) Qabili na Habili.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 21
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kujitolea damu na kumuongezea mgonjwa na kwamba kumuona na kumsaidia mgonjwa ni sababu ya kupatana kwa watu waliokosana, pia imezungumzi umuhimu wa waislamu kuwa kitu kimoja
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 20
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kumsaidia, kumtembelea na kumfariji mtu hasa anapokua mgonjwa, pia imezungumzia namna baadhi ya Waislamu wanavyo ipuuzia na kuisahau Sunna hii
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 19
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa sababu za Allah kumlipa Pepo mtu mwenye kumtembelea mgonjwa na namna ya kumtamkisha mgonjwa kalmia ya laa iLLaha illa LLah, pia imezungumzia umuhimu wa muislamu kujiandaa na kifo
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 18
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: ukamilifu wa mada ilio pita ikizungumzia maana ya kumswalia mtume (s.a.w) kisha amebainisha namna ya kumswalia mtume, na hatari ya uzushi katika dini.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 17
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) juu ya kumtembelea mgonjwa ametaja ubora wa mkutembelea mgonjwa, ikiwemo Malaika elfu sabini wanamuombea dua, na kuzungukwa na rehma, pia imefafanua maana ya malaika kumswalia.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 16
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) juu ya kumtembelea mgonjwa au ndugu katika imani na namna Maswahaba wa Mtume (s.a.w) walivyo dumu na Sunna hii, pia imezungumzia fadhila na malipo yake.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 15
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika kumtembelea mgonjwa, na ubora wake pa amezungumzia hali ya waislam katika zama hizi, na kwamba kumtembelea mgonjwa ni ibada ilio hamwa.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 14
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika namna ya kupiga mswaki, pia imezungumzia umuhimu wa kufuata mwenendo wa Mtume (s.a.w), na ameongelea uwajibu wa usafi na ameendelea kutaja nyakati za kupiga mswaki.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 13
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika taratibu za kupiga mswaki na miongoni mwa faida na tiba inayopatikana katika kupiga mswaki, pia imezungumzia nyakati ambazo ni muhimu na ni Sunna kupiga mswaki.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 12
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kufanya matendo mema kwa siri bila ya kujionyesha mbele za watu, nakwamba ibada za siri nisababu ya kujibiwa dua ikiwa ni kwa ikhlas.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 11
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika umuhimu wa kutoa na kujitolea kwa ajili ya Allah, pia imezungumzia umuhimu wa kuwasaidia masikini na hatari ya ubakhili
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 10
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Aina na dalili za ucha Mungu, nakwamba miongoni mwa dalili za ucha Mungu ni kutumia kitabu cha Alllah na Sunna za Mtume (s.a.w), pia imezungumzia umuhimu wa Muislamu kujiandaa na Akhera.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 09
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mafundisho ya Mtume (s.a.w) katika kufurahishana na kusaidiana mke na mume ndani ya ndoa, pia imezungumzia njia sahihi za kumaliza ugomvi baina ya mume na mke. Kisha ametaja faida za mswaki.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 08
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika kutimiza lengo la ndoa na umuhimu wa wanawake wa kiislamu kumuiga Mama Aisha (r.a), pia imezungumzia umuhimu wa subra kwa wana ndoa.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 07
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika kufanya uadilifu ndani ya ndoa na namna Aisha (r.a) alivyojifakharisha kwa Mtume (s.a.w) wakati wa uhai wake na kabla ya kufa kwake (s.a.w), pia imezungumzia tukio la kufa Mtume (s.a.w).
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 06
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) juu ya nafasi ya usafi katika Uislamu ikiwemo Sunna ya kupiga mswaki, pia imezungumzia ubora na umuhimu wa maisha ya ndoa.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 05
2015-11-10
Mada hii inazungumzia: Dua alizoomba Mtume (s.a.w) ili Allah amkinge na Moto wa Jahanam na Adhabu za kaburini, pia imezungumzia miongoni mwa sababu za watu kuadhibiwa kaburini.
Go to the Top