Kuonyesha Video ( 901 - 925 Katika jumla ya: 1096 )
Sherhu Umdatul Ahkam 08
2015-11-13
Shekh anazungumzia: riwaya ya Imamu shafy kwamba asiye tumia hadithi za Mtume (s.a.w) ni sawa na mkristo, kisha ametaja uwajibu wa kuwachukia wanao kanusha maneno ya Mtume (s.a.w) kisha akataja dalili za kiakili zinazo thibitisha kuwepo kwa hadithi za Mtume (s.a.w).
Sherhu Umdatul Ahkam 07
2015-11-13
Shekh anazungumzia: Itikadi mbaya za wanao pinga hadithi za Mtume (s.a.w) na kwamba wanao pinga hadithi za mtume (s.a.w) ni Mazindiq na ni Mashia, kisha akazungumzia kwa ufupi kuhusu itikadi zao chafu.
Sherhu Umdatul Ahkam 06
2015-11-13
Shekh anazungumzia: Uchafu wa wenye kupinga hadithi za mtume (s.a.w) kisha amenukuu maneno ya Imamu Suyutwiy ambayo yamebainisha hukumu ya mwenye kukanusha hadithi za Mtume (s.a.w) kuwa ni kafiri.
Sherhu Umdatul Ahkam 05
2015-11-13
Shekh anazungumzia: njia za kuifanyia kazi Qur’an kupitia matendo ya Mtume (s.a.w) kisha amebainisha baadhi ya vitabu ambavyo vina warudi wenye kupinga hadithi za Mtume (s.a.w).
Sherhu Umdatul Ahkam 04
2015-11-13
Shekh anazungumzia: Umuhimu wa elimu ya hadithi, kisha amebainisha kwamba asiye amini kuwa hadithi ni hoja basi atakuwa adui wa uislam, kisha amebainisha maana ya kumtii mtume (s.a.w)
Sherhu Umdatul Ahkam 03
2015-11-13
Shekh anazungumzia: Wadhfa wa Hadithi za Mtume (s.a.w) na kwamba zinaweka wazi na kufafanua namna ya utekelezaji wa amri za Qur’an tukufu, pia amezungumza maneno ya Imamu Suyutwi kuhusu cheo cha hadithi za mtume(s.a.w).
Sherhu Umdatul Ahkam 02
2015-11-13
Shekh anazungumzia: Utangulizi wa mtunzi pia amezungumzia Umuhimu wa elim ya hadithi, na maana ya hadithi, na cheo cha Quraan na Sunnah pia amewarudi wenye kuzipinga Hadithi.
Sherhu Umdatul Ahkam 01
2015-11-13
Shekh anazungumzia: Historia fupi ya mwandishi wa kitabu hiki cha umdatul ahkami, Shekh Abdul Ghany Al Maqisy Allah amrehemu, na umuhim wa kuifanyia kazi elim.
Utamu wa ndoa 14
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Sababu za mwanamke kuwa na kiburi katika nyumba, pia imezungumzia hatari kwa mwanamke mwenyekutaka kuwa juu ya mumewe ndani ya ndoa.
Utamu wa ndoa 13
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa mwanamke kutulia nyumbani kwake na kujiepusha na marafiki waovu, pia imezungumzia hatari ya maasi.
Utamu wa ndoa 12
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Utulivu katika ndoa hauwezi kupatika mpaka mume na mke wawe watu wema, pia imezungumzia umuhimu wa mwanamke kujitahidi kumtii na kumridhisha mumewe.
Utamu wa ndoa 11
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Tofauti kati ya wanawake wanaojua majukumu yao na wasiojua, pia imezungumzia hatari ya mwanamke asiyetulia nyumbani kwake mzurulaji
Utamu wa ndoa 10
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa mwanamke kujiepusha na uvivu pamoja na kujitahidi kuamka mapema na kushughulika na taratibu za nyumba yake
Utamu wa ndoa 09
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Hatari ya mume kumdhalilisha na kumtukana mke na kwamba ni muhimu kuchunga mipaka na kumfanyia mazuri mke, pia imezungumzia ubora wa kujiepusha na kuangalia vitu visivyo halali yako.
Utamu wa ndoa 08
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa mambo yanayoleta utamu katika ndoa ni mwanaume kumshukuru mkewe kwa yale mazuri anayomfanyia, pia imezungumzia umuhimu wa wana ndoa kuwa na subra na uvumilivu.
Utamu wa ndoa 07
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa mambo yanayoleta utamu katika ndoa ni wana ndoa kusitiriana kutokana na mapungufu pamoja na kusifiana katika mazuri, pia imezungumzia umuhimu wa kuombana msamaha.
Utamu wa ndoa 06
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa utamu wa ndoa ni mwanamke kujipamba na tabasam pamoja na kumkumbusha mumewe mara kwa mara katika kutafuta rizki ya halali, na ayafanye hayo kwa ikhlas ili kupata radhi za Allah.
Utamu wa ndoa 05
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa tabia nzuri kwa mwanamume ndani ya nyumba, pia imezungumzia umuhimu wa mwanaume kuweka muda maalum kwa ajili ya kukaa nakujumuika na familia yake.
Utamu wa ndoa 04
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Usimamizi wa mwanaume juu ya mwanamke na ubora wa kuisoma ndoa kabla ya kuoa au kuolewa, pia imezungumzia umuhimu wa kumuiga Mtume (s.a.w) katika kutekeleza majukumu ya ndoa.
Utamu wa ndoa 03
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa mambo yenye kuleta utamu katika ndoa ni mwanamke kumtii mumewe, pia imezungumzia ukamilifu wa twaa na faida zake.
Utamu wa ndoa 02
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Aina za mashetani hatari kwa kuvunja ndoa za watu, na kwamba ni muhimu kwa wana ndoa kuchukua tahadhari juu ya mashetani hao, pia imezungumzia miongoni mwa mambo yanayoleta utamu katika ndoa.
Utamu wa ndoa 01
2015-11-13
Mada hii inazungumzia: Utamu wa ndoa, na kwamba ili mtu apate ladha na utamu wa ndoa sharti atafute mwanamke au mwanaume mwema, pia imezungumzia umuhimu kwa wanandoa kusameheana ktk ndoa.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 32
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Mahala atakapo pumzika Mtume (s.a.w) Peponi baada ya kufa kwake, pia imefafanunua na kutafsiri maajabu yote aliyo kutana nayo Mtume (s.a.w) na Malaika.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 31
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) katika hadithi ya ndoto na maajabu aliyoyaona akiwa na Malaika, pia imezungumzia nyumba aliyokabidhiwa Mtume (s.a.w) na Malaika baada ya safari ndefu.
Wito wa Mtume (s.a.w) Katika Mwongozo Wake 30
2015-11-11
Mada hii inazungumzia: Mwongozo wa Mtume (s.a.w) juu ya malipo ya mtu mwenye kuswali swala ya jamaa nyuma ya takbira ya Imamu kwa siku arubaini, pia imezungumzia swafu iliyo bora kwa wanaume.
Go to the Top