Kuonyesha Video ( 926 - 950 Katika jumla ya: 1290 )
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Sababu ya mama Aisha (r.a) kuachwa na msafara na hatimaye kusaidiwa na Swahaba Swaf’wan bin Muwatwal (r.a), pia imezungumzia hatari na maafa ya ulimi.
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Maneno aliyosema mama Aisha (r.a) kabla ya kushuka Aya kwa Mtume (s.a.w) za kumtakasa kutokana na uchafu aliozushiwa, pia imezungumzia hatari ya kumzushia muislamu uchafu wa zinaa na kwamba ni katika madhambi makubwa.
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Mtume (s.a.w) kumruhusu bi Aisha (r.a) kwenda kwao wakati akisubiri suluhisho kutoka kwa Allah kutokana na uzushi aliozushiwa, pia imezungumzia kilio alicholia mama Aisha (r.a) mbele ya wazazi wake.
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Kisa cha uzushi aliozushiwa mama Aisha (r.a) na kwamba madhara ya ulimi ni makubwa kulikoupanga, pia imezungumzia hatari na ubaya wa uzushi katika uislamu.
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa kujifunza na kuiga namna Mtume (s.a.w) alivyoishi na wake zake ili kuzijenga familia katika uislamu wa kweli, pia imezungumzia hatari ya kuvuka mipaka na kuipotosha jamii.
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) bi Aisha bint Abubakar (r.a) ambaye alisifika na sifa ya ujuzi (elimu), pia imezungumzia ubora na nafasi ya bi Aisha (r.a) katika uislamu.
2015-12-08
Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) bi Safia bint Huyay (r.a) ambaye ni mwanamke aliyesifika na sifa ya ukweli, pia imezungumzia mafundisho yanayopatika kutoka katika nyumba ya Mtume (s.a.w).
2015-12-07
Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) bi Hafsa bint Omar bunil-Khatwab (r.a) na kwamba ndio mke wa Mtume (s.a.w) katika pepo, pia imezungumzia mazingatio yanayopatikana katika nyumba ya Mtume (s.a.w).
2015-12-07
Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) Ummu Habiba Ramla bint Abi Sufiyan (r.a), na ukubwa wa imani na msimamo aliokuwa nao, pia imezungumzia sifa walizo kuwa nazo wake wa Mtume (s.a.w).
2015-12-07
Mada hii inazungumzia: Historia fupi ya mke wa Mtume (s.a.w) Zainab bint Jahshi (r.a), na sababu za kuolewa kwanza na Zaid bin Haritha (r.a), pia imezungumzia sababu ya Mtume (s.a.w) kumuoa Zainab bint Jahshi.
2015-12-07
Mada hii inazungumzia: Nafasi ya bi Khadija (r.a) katika Uislamu na umuhimu kwa wanawake wa kiislamu kumuiga bi Khadija (r.a), pia imezungumzia ucha Mungu na uadilifu aliokuanao bi Khadija, na athari aliyoacha baada kufa.
2015-12-07
Mada hii inazungumzia: Wanawake katika nyumba ya Mtume (s.a.w) na imeanza na historia fupi ya bi Khadija (r.a), pia imezungumzia mwanzo wa wahyi (ufunuo) kumshukia Mtume (s.a.w).
2015-12-03
Kwenye mada hii ya video kwa lugha ya Korea inazungumzia Maana ya dini ya Uislamu kwa ufupi.
2015-12-03
Katika muhadhara huu kwa lugha ya kingereza anazungumzia Sheikh Yusuf Estes Uzuri wa Uislamu wa uhakika, na namna Muislamu atavyo kabiliana na vitu vibaya vinavyo tokea ktk uhai huu.
2015-12-03
Kipindi kipya cha sheikh Baba Amina Bilali Filips anaelezea kuhusu wazururaji na wasio kuwa na malengo ya kuwepo kwao ktk maisha haya, na wakitaka hivyo watapotea ktk nja ya sheitwani, kwa sababu hiyo sheikh anatoa nja sahihi mtu akifuata njia hiyo atabainikiwa na haki kutokana na upotovu.
2015-12-01
Muhadhara kwa lugha ya Talga, ukielezea maana ya dini tukufu ya Uislamu, na kwamba ndio dini ya haki na ndio dini ya Mitume wote.
2015-12-01
Katika kipindi hiki ataelezea sheikh Eddie sababu zinazo pelekea wanawake wengi kuingia ktk Uislam kuliko wanamume, na namna walivyo pata uhuru wa kweli na amani ndani ya Uislamu.
2015-12-01
Video hii inaelezea namna Uislamu ulivyo piga vita Ubaguzi kati ya viumbe.
2015-11-27
Mada ya video kwa lugha ya kingereza Sheikh Yusuf Estes kajibu maswali ya mwanamke wa kikristo kwa sababu gani kaacha ukristo na kuingia ktk Uislamu.
2015-11-27
Kazungumza Sheikh kwa lugha ya kingereza kuhusu Uislamu kwa ujumla, kabainisha Mwenyezi Mungu Mtukufu ni nani? Uislamu ni nini? Muhammad (s.a.w), ni nani? mwisho kabisa kajibu maswali.
2015-11-27
Muhadhara unaelezea Uislamu na daraja zake na matunda yake na mazuri yake na vitenguzi vyake.
2015-11-27
Kazungumzia Sheikh mafundisho ya uislamu na mazuri yake na kulingania kwanjia ya ufupi, muhadhara umehudhuriwa na wengi wasiokuwa waislamu.
2015-11-27
Mazuri ya uislamu Sheikh Yusuf Estes Huda TV, mada ya 9: Kuumbwa kwa Nabii Adam (s.a.w), na kisa cha Shaitwani.
2015-11-27
Mazuri ya uislamu Sheikh Yusuf Estes Huda TV, mada ya 8: Imani ktk Uislamu.
2015-11-27
Mazuri ya uislamu Sheikh Yusuf Estes Huda TV, mada ya 7: Kumuamini Allah.
Go to the Top