Kuonyesha Video ( 501 - 525 Katika jumla ya: 1290 )
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Mipango ya makafiri juu ya kuuangamiza uislamu na kwamba ni mipango ya muda mrefu, pia imezungumzia umuhimu wa waislamu kujidhatiti katika vyuo, misikitiki na majumbani ili kuwajenga vijana wa kiislamu katika imani ya kweli.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa mambo yanayofanya imani izidi ni muislamu kudumu katika kuisoma Qur’an tukufu, pia imezungumzia umuhimu wa kufanya da’awa kama walivyofanya Maswahaba (r.a.w).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa elimu na kwamba elimu humfanya muislamu kuwa juu endapo atasoma kwa ajili ya Allah, pia imezungumzia umuhimu wa waislamu kusomea udaktari kutokana na zama tulizo nazo.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Masharti ya kukubaliwa matendo na imefafanua maana ya kufanya jambo kwa ajili ya Allah, pia imezungumzi umuhimu wa kutafuta elimu kwa ajili ya Allah na kuunufaisha umma wa kiislamu.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Uzinduo kwa umma wa kiislamu ili wawajue maadui wa Uislamu na waislamu, pia imefafanua baina ya imani ya kweli na imani mbovu, na kwamba kwa kushikamana na Qur’an imani inakua thabiti.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Ukubwa wa imani waliyoipata wanawake wa kianswari baada ya kushuka Aya za hijabu, pia imezungumzia mfumo na mwongozo wa Qur’an na Sunna za Mtume (s.a.w).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Kuipenda dunia na kuiacha Qur’an tukufu ni katika sababu za kudhoofika umma wa kiislam katika jamii, pia imezungumzia namna gani Maswahaba walivyokuwa wakifundishwa Qur’an na Mtume (s.a.w).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Umuhimu wa imani na sababu za kudhoofika umma wa kiislamu, pia imefafanua maana ya kukihama kitabu cha Mwenyezi Mungu na imezungumzia uzito na thamani ya Qur’an tukufu.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni ule wa kulia machozi nguzo ya mtende wakati Mtume (s.a.w) alipokua akitoa khutba katika Msikiti wa Madina, pia imezungumzia kuwa Mtume (s.a.w) ndiye mwenye miujiza mingi kuliko mitume wote.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Maneno mazito ya Mtume (s.a.w) aliyosema akiwa Arafa katika Hijja yake ya mwisho, alisema ichukueni elimu kabla haijaondoka, pia imezungumzia umuhimu wa kushikamana na Qur’an na Sunna za Mtume (s.a.w).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyoacha amesema ya kwamba wataondoka (watakufa) Wanachuoni na ujinga utadhihiri, pia imezungumzia umuhimu wa elimu na hatari ya ujinga.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni mameno aliyosema kwamba kikikaribia kiyama zama zitakaribiana mwaka utakua kama mwezi, amali zitakua chache na ubakhili utakithiri, pia imezungumzia umuhimu wa kusoma dini.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa watu waliodai Utume ni Milza Ahmadi Alkaadiyan aliyedai kwamba anapata wahyi kutoka mbinguni, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.a.w) aliposema kwamba utakithiri ujinga katika zama hizi na elimu itashuka.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa watu waliodai utume baada ya kufa Mtume (s.a.w) ni mwanamke aitwae Sajjaha bintul-Harith, na wengineo.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyosema kwamba hakitosimama kiyama ila watatokea watu waongo watakaodai Utume, pia imezungumzia vita aliyopigwa Musailama Al-kadhaab baada ya kudai Utume.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni mambo ya shari aliyomwambia Swahaba Hudhayfa bunil-Yamany (r.a) kwamba yatatokea katika zama hizi, pia imezungumzia ushauri na wasia wa Mtume (s.a.w) kwa Hudheyfa (r.a).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni kwamba mambo aliyoacha amesema kuwa yatatokea zama hizi yamesha tokea, pia imezungumzia umuhimu kwa waislamu kufanya bidii katika kutenda matendo yaliyo mema.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyosema wakati wa uhai wake Mtume (s.a.w) na yakatokea baada ya kufa kwake, miongoni mwa hayo ni maneno aliyosema kwamba zitakuja zama za fitna na watu watauana sana.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni muujiza uliotokea kwa Abuu Jahli alipotaka kumdondoshea jiwe Mtume (s.a.w) wakati akiswali, lile jiwe likamng’ang’ania mikononi, pia imezungumzia muujizaa Mtume (s.a.w) uliotokea kwa Fudhwaala bin Ubaad (r.a).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni maneno aliyombashiria mwanae Fatwima (r.a) kwamba baada ya kufa Mtume (s.a.w) yeye ndiye atakaekuwa wa kwanza kumfuata katika familia yake, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.a.w) kwa Abuu Jahli baada kumdhulum mtu ngamia.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni Muujiza uliotokea kwa Khaatwib bin Abi Balta’a (r.a) alipoandika barua na kuituma Mkka ili kutoa siri ya kivita, Mtume (s.a.w) akajua kabla barua haijafika Makka.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni kuzungumzia mambo ambayo ni ya ghaibu kama alivyo wabashiria Maswahaba pepo na kuwaeleza fitna zitakazo wapata waka wa ukhalifa, pia imezungumzia umuhimu wa muislam kujiepusha na fitna.
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni kwamba aliyomuombea dua Qaisi bin Zaidi (r.a) kisha akapangusa kichwa chake sehem ile aliyoigusa Mtume (s.a.w) haikuota mvi mpaka anakufa, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.w.a) kwa Abuu Hurera (r.a).
2016-03-09
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni muujiza uliotokea kwa Ummu Maabad wa kutoa maziwa katika mbuzi asiye na maziwa, pia imezungumzia namna Mtume (s.a.w) alivyosafishwa na Allah.
2016-03-08
Mada hii inazungumzia: Miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w) ni muujiza wa kutemea mate katika kisima cha Anasi bin Maliki (r.a) maji yale yakawa matam kuliko visima vote vya Madina, pia imezungumzia muujiza wa Mtume (s.a.w) kwa Ukasha (r.a) wa kubadilisha mti kugeuka upanga vitani.
Go to the Top